Ufugaji Bora wa Kuku wa Kienyeji – Part 2
KUZALIANA NA KUTOTOLESHA >> Uchaguzi wa Kuku bora Ili upate kundi lenye kuku bora huna budi uchague jogoo bora na matetea bora wa kuzalisha kundi lako. Angalia sifa zifuatazo unapochagua: i. Tetea na jogoo wawe na umbo kubwa. ii. Wanaokua haraka. iii. Wenye uwezo wa kustahimili magonjwa. iv. Matetea wanaoweza kutaga mayai mengi v. Matetea wanaweza kuatamia na hatimaye kutotoa vifarangakwa wingi na kuvilea vi. Jogoo unaowachagua kwa ajili ya matetea au makoo yako wasiwe na uhusiano wa damu. Ukiishachagua wazazi wa kundi lako changanya jogoo na matetea kwa uwiano wa jogoo mmoja kwa matetea 10 hadi 12. Ukiwa na matetea 20 utahitaji kuwa na jogoo wawili. Nchini kwetu zipo aina tofauti za kuku wa asili ambao wana sifa tofauti. Wafugaji wengi hufuga kutegemeana na uwezo wa kuku kuhimili magonjwa ,kuwa na uzito mkubwa, utagaji wa mayai mengi n.k. Koo za kuku wa asili wenye sifa za namna hii ni aina ya Bukini , Kuchi, Kuchere na wa Kawaida wasio na ukoo maalum. Hawa kwa ujumla wao ...