Ugonjwa wa Mnyauko wa migomba (Banana bacterial wilt)
MUHTASARI Ugonjwa wa Mnyauko bakteria wa migomba (Banana Xanthomonas Wilt, BXW) umepewa jina lake kutoka kwa bakteria wanaoambukiza na hatimaye kuua mgomba. Ugonjwa huo umeongezeka sana nchini Tanzania tangu ulipogundulika kwa mara ya kwanza mwaka wa 2006 mkoani Kagera ukutokea nchini Uganda. Aina zote za migomba hushambuliwa ingawa matokeo ya utafiti yameonyesha uwezekano wa kupatikana kwa aina sugu siku zijazo. Aina kuu ya usimamiaji kwa sasa ni kuzingatia usafi wa shamba: kupanda mazao ya afya, kutumia zana safi za kukatia na kuondoa maua dume ili kupunguza kuathiriwa kupitia wadudu wanaobeba bakteria wakati wanapofyonza utomvu. VISABABISHI Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria Xanthomonas campestris pv. musacearum . ‘pv.’ husimamia kwa neno pathovar na inaonyesha aina fulani ya X. campestris ambayo huambukiza tu migomba pekee na jamii yake ya karibu ya ensete. Hapo awali ilikuwa inajulikana kama X. musacearum . Bakteria wanaweza kuenea kwa njia ya wadudu wanaotembe...