UVUNAJI Zao la ndizi huweza kuanza kuvunwa katika kipindi cha miezi 9 hadi miezi 15 tangu kupandwa kwa chipukizi. Muda wa kuvunwa hutegemea hali ya hewa. Katika sehemu za joto ndizi huvunwa mapema zaidi kuliko sehemu za baridi. Pia migomba iliyopandwa kwa kutumia machipukizi huzaa mapema kuliko iliyopandwa miche iliyozalishwa kwa chupa (tissue culture). MATUMIZI YA RIBONI Riboni za rangi moja (au alama ya kamba) hufungwa kwenye migomba ya umri mmoja mara tu inapoanza kuchanua, na riboni ya rangi nyingine hufungwa kwenye migomba itakayoanza kuchanua wiki mbili hivi zinazofuata na kuendelea hivyo ili kurahisisha kuitambulisha mikungu ambayo itavunwa kwa wakati mmoja. Pia matumizi ya riboni hurahisiha utunzaji wa kumbukumbu ili kujua ni lini na ni mikungu mingai itavunwa. WAKATI UNAOFAA KUVUNA Mkungu wa ndizi huweza kuvunwa katika hatua tofauti kulingana na matumizi, aina na mahitaji ya soko. Mkungu huachwa kwenye mgomba mpaka vidole (matunda ) vimejaa. Uzito wa mkungu hongezeka hara...
Bodi ya Ushirika wa Wakulima Wadogowadogo wa Kilimo cha Umwagiliaji mpunga Dakawa Ltd inatangaza nafasi ya ajira ya Meneja wa shamba katika mashamba 10 ya mpunga Dakawa. Majukumu ya meneja wa shamba (Farm Manager) 1. Kusimamia shughuli zote za uzalishaji katika msimu kwa kuzingatia kalenda 2. Kuandaa kalenda ya umwagiliaji (Irrigation scheduling) kwa kila msimu 3. Kuhakikisha wakulima wanapanda mazao yaliyoidhinishwa msimu husika 4. Kuratibu shughuli za umwagilioji katika skimu 5. Kuandaa mpango kazi na kusimamia ukarabati wa miundombinu ya umwogiliji katika skimu 6. Kuandaa na kusimamia matumizi bora ya zana za kilimo 7. Kuhakiki na kusimamia matumizi ya mbolea na viuatilifu 8. Kusimamia na Kuratibu maswala ya mazingira katika skimu 9. Kuandaa ripoti ya mwezi, robo, nusu, robo tatu mwaka na mwaka mzima 10. Kuandika no kutunza kumbukumbu za vikao vya bodi (Atakuwa katibu wa Bodi) 11. Kushirikiana na Bodi katika kuandaa mipanga ya maendeleo ya muda mfupi na ya muda mrefu 12. Kuandaa ta...
Comments
Post a Comment