Posts

Showing posts with the label NYANYA

Wadudu waharibifu wa nyanya na dawa zake

Image
Ili uweze kubaini mapema uwepo wa wadudu waharibifu au magonjwa katika mimiea yako ya nyanya ni lazima uwe unachunguza mimea yako mara kwa mara. Angalia uwepo wa wadudu kwenye sehemu ya chini ya majani, juu yake, kwenye mashina, maua au matunda kama yametobolewa au la. Sasa ungana nami katika makala hii uweze kujua ni wadudu wepi waharibifu kwenye zao lako la nyanya shambani kwako ili uweze kukabiliana nao. Pia waweza kujua magonjwa ya nyanya na dawa zake hapa 1.   Funza wa vitumba: American bollworm ( Helicoverpa armigera ) Kubaini mapema mayai au funza kabla hayajatoboa matunda ni muhimu sana. Funza wachanga kwanza hula majani baadae matunda. Funza wakishaingia ndani ya matunda husababisha uharibifu mkubwa. Uharibifu kwenye matunda machanga husababisha kupukutika kwake, wakati mashambulizi ya matunda yaliyokomaa husababisha matundu ambayo huruhusu kuingia kwa aina nyingine za ukungu na bakteria ambao huleta madhara zaidi. Funza wa vitumba anavyotoboa nyanya Kipepeo chake huwa na...

Magonjwa hatari ya nyanya na dawa zake

Image
Pamoja na umuhimu wa zao la nyanya, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Sasa ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato lake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili la nyanya. Utangulizi Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa  na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida  na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu  wa zao hili.  Katika makala hii tutaangalia namna ya kudhibiti baadhi ya magonjwa na wadudu  muhimu wa zao la Nyanya. 1. Ugonjwa wa Ukungu (i) Bakajani tangulia au ukungu mapema: Early blight ( Alternaria solani) Dalili Dalili za ukungu mapema hutokea kwenye matunda, shina, na majani ya nyanya. Majani huonesha madoa ya kahawia ...