Posts

Showing posts with the label FARMING

Jinsi ya Kuandaa Mbegu Ya Uyoga

Image
MAHITAJI : Unatakiwa kuwa na : Ø Chumba maalumu kisichopitisha mwanga Ø Presure cooker au jiko maalumu lenye moto mkali Ø Vyombo vya kuwekea mbegu kama vile glass Ø Maji salama Ø Ungaunga wa viazi vitamu Ø Uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu Ø Kibakuli kidogo chenye mfuniko na Ø Kipande cha uyoga (ambacho kitachanganywa na maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu, kwa ajili ya kutengeneza fangasi ambao watatumika kutengeneza mbegu ya uyoga) HATUA YA KWANZA: Kuandaa fangasi 1. Changanya kipande cha uyoga na maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu, kwa ajili ya kutengeneza fangasi ambao watatumika kutengeneza mbegu ya uyoga) 2.  Baada ya kuchanganya  mchangnyiko huo, chemsha mchanganyiko huo kwenye presha cooker au jiko la moto mkali. 3.  Ipua na weka mchanganyiko huo kwenye vibakuli vidogo vinne vyenye mfuniko 4.  Acha...

Kilimo Cha Matikiti Maji Kisasa

Image
" Kilimo cha matikiti huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0 " Utangulizi Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuri za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine (curcubitaceae family) kama matango, maboga na maskwash (squash). Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi. Katika shamba la ukubwa wa ekari moja (1 acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvu...

Jifunze Kilimo Bora Cha Uyoga

Image
“ Mbegu za uyoga huzalishwa kwenye maabara zenye vifaa vinavyowezesha kuotesha mbegu hizo bila kuchafuliwa au kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii nyingine za uyoga ambazo haziliwi. Hapa Tanzania hivi sasa maabara hizo zipo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kituo cha utafiti wa kilimo-Uyolena taasisi ya utafiti wa kilimo cha bustani- Tengeru (HORTI – Tengeru, Arusha). ”   Utangulizi Miaka ya karibuni, utaalamu wa kilimo cha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, urahisi wa teknologia ya kuotesha katika mazingira ya Tanzania na soko lake kwa wananchi na katika hotel. Hata hivyo ni wananchi wachache tu wanaojua kilimo cha uyoga. Uyoga unaozalishwa unafahamika. Aina zinazofaa kwa Tanzania ni zile ambazo hustawi ...

Kilimo bora cha Viazi Vitamu (Sweet potatoes)

Image
  “Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi kupenya na kupanuka.” Utangulizi Kilimo cha Viazi Vitamu ni muhimu sana kwani viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi katika jamii ya ki-Tanzania. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Viazi vitamu asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro, Kagera, Arusha na Ruvuma. Matumizi Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati, tambi na Juice. Majani ya viazi huliwa kama mboga (matembele) pia hutumika katika kutayarisha mboji. Aina Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinaz...