Kilimo cha zao la vanilla - part 2
Katika kipindi kilichopita tuliona mahitaji ya zao la vanilla na jinsi linavyolimwa , sasa leo napenda kukukaribisha ndugu yangu mkulima katika sehemu hii ya pili ambapo tutaona: magonjwa na wadudu waharibifu wa zao la vanilla likiwa shambani pamoja na kuvuna, kukausha na soko lake. Karibu... MAGONJWA, WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU Mmea wa vanilla kwa kawaida haushambuliwi mara kwa mara na magonjwa au wadudu waharibifu kama shamba limetunzwa vizuri. Mashambulizi ya magonjwa na wadudu waharibifu ni dalili ya utunzaji duni wa shamba. Ili kuepuka hali hiyo, ni muhimu kukagua shamba kila wakati kubaini na kurekebisha yafuatayo: Nafasi kati ya mmea na mmea ni ya kutosha kuruhusu mzunguko wa hewa safi na hivyo kupunguza hali inayoruhusu vimelea vya magonjwa kuishi na kuzaliana. Kivuli kisiwe kizito ili kuepuka giza linalowavutia wadudu waharibifu na kuruhusu vimelea vya magonjwa. Kivuli chepesi husababisha kuungua kwa majani na kufanya mmea kutokua vizuri Afya ya mmea ikaguliwe kwa...