Posts

Showing posts with the label MAZAO YA VIUNGO

Kilimo cha Pilipili Mtama

Image
Pilipili  mtama  au kwa jina lingine pilipili  manga ni kiungo muhimu sana katika mapishi. Radha yake ya muwasho ndio kitu hasa kinachotafutwa katika vipunje vidogo vidogo vya zao hili. Pilipili manga husagwa ili kupata ungaunga kabla ya kutumika ingawa pia inaweza kutumika bila kusagwa. UTANGULIZI Jina la kitalaam ni Piper nigram na kwa kiingereza ni black pepper . Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar. Ingawa pia inaweza kukubali katika maeneo ya Kagera Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi za magharibi zina matumizi makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi ndiyo huzalishwa zaidi hapa nchini. UZALISHAJI • Hali ya hewa na udongo Viungo vingi humea katika maeneo yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 24-26 na huzalishwa maeneo ya mwambao. Udongo wenye rutuba na unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5. Mahitaji ya mvua n...

Kilimo cha zao la vanilla - part 2

Image
Katika kipindi kilichopita tuliona  mahitaji ya zao la vanilla na jinsi linavyolimwa , sasa leo napenda kukukaribisha ndugu yangu mkulima katika sehemu hii ya pili ambapo tutaona: magonjwa na wadudu waharibifu wa zao la vanilla likiwa shambani pamoja na kuvuna, kukausha na soko lake. Karibu... MAGONJWA, WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU Mmea wa vanilla kwa kawaida haushambuliwi mara kwa mara na magonjwa au wadudu waharibifu kama shamba limetunzwa vizuri. Mashambulizi ya magonjwa na wadudu waharibifu ni dalili ya utunzaji duni wa shamba.  Ili kuepuka hali hiyo, ni muhimu kukagua shamba kila wakati kubaini na kurekebisha yafuatayo: Nafasi kati ya mmea na mmea ni ya kutosha kuruhusu mzunguko wa hewa safi na hivyo kupunguza hali inayoruhusu vimelea vya magonjwa kuishi na kuzaliana. Kivuli kisiwe kizito ili kuepuka giza linalowavutia wadudu waharibifu na kuruhusu vimelea vya magonjwa. Kivuli chepesi husababisha kuungua kwa majani na kufanya mmea kutokua vizuri Afya ya mmea ikaguliwe kwa...

Kilimo cha zao la vanilla - part 1

Image
Zao hili lilianza kuingia nchini kutoka Uganda mnamo mwaka 1954 kupitia kwa mkulima mmoja wa kijiji cha Kiilima wilaya ya Bukoba Vijijini. UTANGULIZI Zao la vanilla ni moja ya zao la viungo ambalo asili yake ni Kusini Mashariki ya Mexico na sehemu nyingine za Amerika ya Kati. Vanilla hulimwa katika nchi mbalimbali duniani. Nchi zinazolima kwa wingi ni pamoja na Madagascar, Comoro, Tahiti, Uganda, India na nchi nyingine za Amerika ya Kati. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazolima vanilla katika Afrika. Zao hili lilianza kuingia nchini kutoka Uganda mnamo mwaka 1954 kupitia kwa mkulima mmoja wa kijiji cha Kiilima wilaya ya Bukoba Vijijini. Vanilla imeanza kulimwa kibiashara hasa katika mkoa wa Kagera mwaka wa 1992.  Katika mkoa wa Kagera, kilimo cha Vanilla kimehamasishwa zaidi na Chama cha Maendeleo Ya Wakulima kinachofahamika kama MAYAWA. Chama hiki kimekuwa kikihimiza uzalishaji na usindikaji wa Vanilla ambayo huuzwa kupitia kampuni zilizopo Uganda. Mmea wa Vanilla huzaa maharage ...

Kilimo cha Viungo Chachu ya Uchumi Morogoro

Image
Milima ya Uluguru-Morogoro ASILIMIA 90 ya wananchi katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ni wakulima na wamekuwa wanakitumia kilimo kujiendeleza kiuchumi, wao na halmashauri hiyo. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 halmashauri hiyo inakadiriwa kuwa na watu 286,248. Kilimo cha mazao ya chakula na biashara licha ya kuwanufaisha wakulima pia ni chanzo cha makusanyo ya mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro . Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Yona Mark, anasema, ardhi katika halmashauri hiyo imegawanyika kiuzalishaji kwa mazao ya chakula, matunda na kibiashara. Anasema kwamba halmashauri hiyo ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 11,925.75 ambazo ni sawa na hekta 1,192,575 na kwamba, eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 447,000. Mark anataja eneo linalotumika kwa uzalishaji kwa kilimo na wakulima wadogo ni hekta 78,794.96 na jumla ya mashamba 63 yana hati miliki. Anasema eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta 28,075 , na kwamba he...