Posts

Vitunguu - Kilimo na Hifadhi Bora. Part 2

Image
3.0 KUVUNA NA HIFADHI YA VITUNGUU Kabla ya kuvuna vitunguu kagua shamba ili kuhakikisha kuwa vitunguu vimekomaa. Dalili ya vitunguu kukomaa ni:- · Majani kunyauka na kuanza kukauka · Asilimia 75 -100% kuangusha shingo na majani kukauka. Soma KILIMO CHA VITUNGUU Part 1 3.1 KUVUNA Viitunguu huweza kuvunwa siku 90 mpaka 150 tangu kupanda mbegu kutegemeana na aina. Vitunguu vinavunwa kwa mikono. Mimea inang’olewa au kuchimbuliwa kwa kutumia rato (jembe uma). Baada ya kuvuna vitunguu vinaweza kuachwa shambani vikiwa vimefunikwa na majani kukinga jua kali kwa muda wa siku mbili au tatu kutegemeana na hali ya hewa. Lengo ni kuimarisha ngozi ya vitunguu na kufanya michubuko na majeraha madogo madogo yanayotokea wakati wa kuvuna kuwa magumu na kutengeneza mokovu ambayo yanazuia vimelea vya magonjwa kuingia ndani. Pia kupunguza unyevu kwenye majani na mashina na kuruhusu sehemu ya chini ya shingo kufunga. Ikiwa usalama ni mdogo, vitunguu vinachambuliwa na kukatwa majani na mizizi na kuanikwa se...

Magonjwa na Wadudu Waharibifu wa Vitunguu

Image
Vitunguu vinashambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali na kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Ili kudhibiti tatizo kwanza shamba likaguliwe mara kwa mara kuona dalili za mashambulizi. MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU WA VITUNGUU Vitunguu vinashambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali na kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Ili kudhibiti tatizo kwanza shamba likaguliwe mara kwa mara kuona dalili za mashambulizi.  Endapo kuna dalili za mashambulizi, chukua hatua za kuzuia kabla uharibifu mkubwa haujatokea. Soma KILIMO CA VITUNGUU Part 1 MAGONJWA YA VITUNGUU a) Baka zambarau (Puple Blotch) Ungonjwa huu unasababishwa na kuvu (fangasi). Chanzo kikubwa cha ugonjwa ni mbegu zenye ugonjwa. Pia ugonjwa unajitokeza wakati kuna ukungu na unyevunyegu mwingi hewani has wakati wa masika. Kiasi cha 60-80 % ya mazao yanaweza kupotea kama ugonjwa hautadhibitiwa. Dalili za ugonjwa ni:- · Kujitokeza madoa meupe yaliyodidimia kwenye majani na kwenye mashina ya mbegu · Rangi ya zambarau kuwepo ...