"Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzoni mwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1 st to 15 th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni...." KUANDAA SHAMBA, KUPANDA NA KUPALILIA 1. Kuandaa Shamba, Kusafisha, Kulima/Kutifua Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa. Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia: i). Jembe la mkono - wengi wanatumia ii). Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe iii) . Power tillers iv). Matrekta Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la kukokotwa na wanyama yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na kuufanya kuwa tif...
....kutokana na mavuno ya soya, mkulima anaweza kupata mapato mengi ukilinganisha na mazao kama mahindi na maharage kwa eneo lililosawa na eneo la soya. Ukweli huu unabainishwa na tathmini iliyofanyika mwaka wa 2005 na Wizara ya Kilimo na Chakula, juu ya hali kilimo cha soya nchini. 4. WADUDU, MAGONJWA NA WANYAMA WAHARIBIFU Wadudu Wadudu mafuta (Aphids) Kwa sasa, nchini Tanzania soya haishambuliwi sana na wadudu kama ilivyo sehemu nyingine ambako zao hilo hulimwa kwa wingi. Hata hivyo endapo wadudu watatokea mkulima anashauriwa kutumia dawa za wadudu kama Thiodan 35% EC na Sumithion 50% EC kwenye kipimo cha mililita 40 za dawa na lita 20 za maji au kipimo kinacho pendekezwa katika dawa husika. Upuliziaji wa dawa ufanywe kulingana na kiasi cha mashambulizi ya wadudu kwenye mazao. Tofauti na mazao kama mahindi na maharage, hakuna wadudu waharibifu wa soya ghalani. Hivyo zao hilo linaweza kutunzwa kwa muda mrefu ghalani bila kuwa na athari za wadudu. Kwa mkulima na wafanyabiashara, kuto...
“ Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18 °C hadi 35 °C. ” Utangulizi Nanasi ni tunda la kitropiki, linapendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma. Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi. Hali ya hewa Kilimo c...
Comments
Post a Comment