Mahitaji ya Udongo na Mbolea katika kilimo cha Mahindi
Habari, na karibu tena katika muendelezo wa mafunzo yetu ya kilimo cha kisasa. Leo tutaangazia kwenye mahitaji ya Udongo na Mbolea katika kilimo cha Mahindi. Karibu … Mahitaji ya udongo na mbolea ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mmea wowote ule, hata hivo mahitaji hayo hutofautiana kati ya mmea moja na lingine kutokana na kutofautiana kwa sehemu ya zao (product) katika hiyo mimea (yaani economic part of a plant). Kwa mfano: mahindi, mpunga sehemu ya zao ni mbegu/punje, wakati nyanya, na bilinganya zao lake ni tunda nakadhalika viazi zao lake ni mizizi! Hivyo basi mahitaji ya udongo na mbolea katika kilimo cha mahindi ni tofauti na mazao mengine, endelea.... UDONGO Udongo una rutuba ya asili yaani virutubisho katika udongo, mboji (organic matter) , na viumbe mbalimbali vinavyoishi kwenye udongo. Rutuba ya udongo inategemea sana hali ya udongo kikemia, kibiolojia na kifizikia. Makundi Ya Udongo Kuna makundi makuu matatu ya udongo, kutokana na ukubwa wa c hengachenga za udong...