“ Kilimo cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji wa nanasi kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18 °C hadi 35 °C. ” Utangulizi Nanasi ni tunda la kitropiki, linapendwa na walaji wengi kwa sababu ya ladha yake tamu na harufu yake nzuri. Tunda hili laweza liwa mara tu baada ya kuvunwa, baada ya kulipika, au kama juisi. Nanasi ni chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini chuma. Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi. Hali ya hewa Kilimo c...
Comments
Post a Comment